Nilikua kwenye halaiki Yesu alipokufa. Nikamuona alivyoning'inia, Mwokozi wangu Nikaliona taji la miba, na vijito vya damu yake. Huyu ndiye tabibu wetu, Sasa mmemfanyia nini Nikajitosa miguuni na kwa hasira nikaita. Ni nani kamtundika hapo juu, mtoto wa amani? Ni nani kamtundika hapo juu? Jitokeze unikabili Ni nani kamtundika hapo juu? Na halaiki ikanichekelea nikageuka nikaiona nyundo mkononi mwangu Ni Nani kamtundika hapo juu? Mtoto wa amani Mimi mwanajeshi wa kirumi, mtu wa kawaida. Nina mpenzi na watoto wangu. Najikaza tu Ni vipi ningemuua Yesu? Kweli kuna mtu mwingine. Siwezi beba hizo lawama. Kuna kuchanganyikiwa hapa Siwezi kuwa mshukiwa. Ni lazima mniambie Ni mimi niliyemtundika Juu, mtoto wa amani Ni mimi niliyemtundika juu. Ndimi mshukiwa mkuu. Ni mimi niliyemtundika juu kwa dhambi hata na maasi yangu. Mwenye imani ninapoasi nampiga nyundo tena (2)