Muziki asili yake wapi eeeee Muziki ni wa nani eeeee Muziki hakuna mwenyewe Muziki ni mwito Muziki ni fundisho Muziki maombolezo kilio Usinione nikiimba Ukadhani ninayo furaha Kumbe ninayo huzuni moyoni Muziki alivyo na nguvu ulimwenguni kote Hata makanisani wanaimba kwaya kwa kumuomba Mungu Kumuabudu Mungu Kwa kumsifu Mungu Hata kukiwa sherehe za serikali,mbele ya Mwenyekiti kuhutubia Ni Muziki unaanza kuwakusanya watu Kumbuka Paulo na Sila waliimba gerezani Mungu amewasikia Kumbuka Musa aliimba Muziki wa aina yake Kuwakomboa wana wa Israeli Waliopo utumwani katika nchi ya Misri Kukiwa na sherehe utaimba nyimbo za furaha Kukiwa na tabu utaimba nyimbo za masikitiko Ukifa leo utapelekwa kaburini na nyimbo za maombolezo Ni muziki pekee ulio na nguvu Utawakusanya wabaya na wazuri msiku ya mwisho Mungu akitoa hukumu Muziki sio uhuni Kama muziki ni uhuni kwa nini unanunua kaseti Kama muziki ni uhuni kwa nini unaomba nyimbo redioni Kama muziki ni uhuni kwa nini kwa nini unanunua rekodi Kama muziki ni uhuni kwa nini unacheza muziki weeee Kama muziki ni uhuni kwa nini unafanya top ten show Kumbuka siku ya mwisho ikifika Kutakuwa mlio mmoja wa parapanda utawakusanya wateule wote Walioteuliwa katika pembe nne za dunia Siku ya mwisho Mungu akitoa hukumu,hukumu,hukumu Hata kwa Mungu malaika wanaimba ooh Muziki asili yake wapi eeeee Muziki ni wa nani eeeee Muziki hakuna mwenyewe Muziki ni mwito Muziki ni fundisho Muziki maombolezo kilio Usinione nikiimba Ukadhani ninayo furaha Kumbe ninayo huzuni moyoni Muziki asili yake wapi eeeee Muziki ni wa nani eeeee Muziki hakuna mwenyewe Muziki ni mwito Muziki ni fundisho Muziki maombolezo kilio Usinione nikiimba Ukadhani ninayo furaha Kumbe ninayo huzuni moyoni