Baba yangu, Uliye mbinguni, Naomba unigange moyo, Uniponye afya yangu baba, Na roho wako baba nijaze (Ni kweli Bwana wewe ni mkuu) Uweza wako ni wa ajabu, (Matendo makuuu mimi nayaona) Kwa kweli Bwana wewe ni mkuu Sikufaa kuitwa mwanao Ila ni kwa neema yako tuu Roho yangu naiweka kwako, Maisha yangu Bwana tawala Mwili wangu nauweka kwako, Uwe chombo kikutumikie, Nimechoshwa na dunia hii, Msaada wako nahitaji Kwa kweli Bwana wewe ni Mkuu (Ni kweli) Kwa kweli Bwana wewe ni mkuu (Nimejua) Kwa kweli Bwana wewe ni Mkuu.