Kishore Kumar Hits

MwanaFA - Sio Kwa Ubaya lyrics

Artist: MwanaFA

album: Sio Kwa Ubaya


Falsafaa
Konde boy call me number one
Falsafa baba

Gachi B
Hela sio matako kwamba kila mtu anazo
Zilipo Mwanangu usilete Mchezo
Kuwaza Hela Hakuna Kwenda Likizo
Hasa wenzangu na mimi
Ambao hatukuzaliwa nazo
Eti hazileti furaha ukiwa sikiliza shauri yako
Sio swala la mjadala hii ndo iwe ramani yako
Eeeh pambana ziwe zako
Pigana mwana mpaka wachange jina lako
Tunawatolea sadaka sadaka tunazopata
Laana zinatuepuka dua mbaya zinaturuka
Hata ufahamu kwanini wananiita baba
Roho tisa kama za paka I'm ma brothers keeper
The white collar Don kama Paul Castellano
Wanatangulia kufunga ila sipotezi mapambano
Usiende mbali kumbuka kuna kurudi
Mayai yote kapu moja man karibu unabugi
Moyo wa Champion sioni competition
Mitihani ya maisha hufaulu kwa kwenda tuition
AKA ya ulimwengu
Ninayekutia fimbo za ugoko
Ka hukufunzwa na mama ako
Shauri yako
Mi sina time ya kupoteza
Ngoma ya mtu siwezicheza
So usiponiona usiulize
Jua tu niko bize
Nazichanga si kwa ubaya
Mi sina time ya kupoteza
Ngoma ya mtu siwezicheza
So usiponiona usiulize
Jua tu niko bize
Nazichanga si kwa ubaya

Ukiwa na siku ya kutafuta na ya kupata ipo
Ridhiki hatoi baba ako kwamba itakufuata ulipo
Nakutia moyo kukata tamaa mwiko
Sio lele mama ilibidi mnagombea fito
Penda hela usiziabudu usivukwe na utu
Roho yako ya chuma usiache iwe kutu
Sheria msumeno lakini haichani dhiki
Mawe yameiva na mkaa bado umebaki
Pesa hainunui furaha ufukara unanunua nini
Mi nakimbiza hela mademu mewaachia nyinyi
Hizi si habari za mjini ni habari zangu mimi
Maisha hayana subtitle sio lazima uniamini
Pata hela maadui zako wanune
Usihofu life manigga mipunga ndo nguvu za kiume
Au uendelee kulala ka utakuwa ulichokiota
Asiye hustle na asile ukija kitaa utatukuta
Moyo wa Champion sioni competition
Mitihani ya maisha hufaulu kwa kwenda tuition
AKA ya ulimwengu
Ninayekutia fimbo za ugoko
Ka hukufunzwa na mama ako
Shauri yako
Mi sina time ya kupoteza
Ngoma ya mtu siwezi cheza
So usiponiona usiulize
Jua tu niko bize
Nazichanga si kwa ubaya
Mi sina time ya kupoteza
Ngoma ya mtu siwezi cheza
So usiponiona usiulize
Jua tu niko bize
Nazichanga si kwa ubaya
Kwanza naamka mapema kama naishi Kigamboni
Dili isiyo na pesa Konde Boy humuoni
Gari imefuka moshi
Ka nimepaki jikoni
Na usipumuona Mudi Mnyama
Bunduki ipo kiunoni yeeeh
I go for the money mura
Mi am go for the money money mura
I go for the money mura
Na sina time ya utani utani mura

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

Similar artists