Hakuonekana na binti hakuwahi kuiasi dini Mfuasi mzuri wa maadili (lakini alikufa kwa ngoma) Aliwarudisha waliopotea akawapa tiba mbadala Na adui mkubwa wa zinaa (lakini alikufa kwa ngoma) Najaribu kumjengea picha mshkaji alie kalala ndani ya futi 6 Namkumbuka mtaani mtaani alipokuwa anakatisha Na mara kadhaa maskani washkaji ungemkuta Usingedhani ana ngoma machoni alivyokuwa mwema Mzuri, mtanashati aliyewaza kabla ya kusema Ibilisi wa njaa za mwili daima alimchezea mbali Tungi, vicheche, mineli hakuonekana kujali Tazama maisha yake hutaliona kosa lake Kama aliyefunga kufuli kati kati ya nyeti zake Mkali wa ushauri nasaha aliyeongea kuhusu mapenzi huku akipinga zinaa Ungesema achague kipindi angechagua njia panda Nyumba aipendayo angechagua ya ibada Utepe mwekundu mpaka kwenye nguo zake za ndani Nadhani mimi najali wewe je? Kama alikufa kwa ngoma jiulize alijali nini? Hakuonekana na binti hakuwahi kuiasi dini Mfuasi wa maadili iiih (Lakini alikufa kwa ngoma) Alirudisha waliopotea akwapa tiba mbadala Adui wa zinaa iiih (lakini alikufa kwa ngoma) Mara nyingi alikuwa mpole Mara chache alizoongea wote tulimgeuza shule Nasaha za bure kama tupo class vile Akatuasa kuhusu kuhusiana Akatuonya kutoaminiana Mtazamo wake na wa-mama Terry daima ulifanana Hadithi ya maisha yake ilikuwa safi kama ya Nabii Hakuna aliyeamini mwisho wa mshkaji utakuwa namna hii 'Gawa sana condom na kufunza kama angaza Vijarida vya Ukimwi ye'ndio alikuwa msambaza Ina maana alikuwa anatoa bila vyake kubakiza Ama amekuwa ufunuo mola anaonyesha miujiza Tazama siku zinakata hatumuoni nini kasoro Afya yake haieleweki eti imeanzisha mgogoro Leo anadunda kesho mgonjwa na hataliacha godoro Labda alifanya kwa siri hadharani hakuna shahidi Labda alivumilia sana mwisho kuasi kukambidi Ama ilikua kama ajali kama aliepigwa na radi Hatujui! hatuwezi sema Na bado tunashangaa Vipi vipimo vinasoma Mshkaji alikufa kwa ngoma Hakuonekana na binti hakuwahi kuiasi dini Mfuasi wa maadili iiih (Lakini alikufa kwa ngoma) Alirudisha waliopotea akwapa tiba mbadala Adui wa zinaa iiih (lakini alikufa kwa ngoma) Sijaribu kuibadili nyekundu kuwa njano huu ni mfano Kwamba Ukimwi ni kwa wote Wembamba na wacheza sumo Wazinzi, wema pia wamo na hauji kufuata kimo Ungedhani yupo salama kuzidi usalama wenyewe Ungedhani ukimwi utaogopa utamuacha mshkaji mwenyewe Sivyo! Haufanyi utakavyo wewe Unafanya utakavyo wenyewe Hakuonekana ana binti hakuwahi kuiahasi dini Mfuasi mzuri wa maadili "Lakini alikufa kwa ngoma" Amewarudisha walopotea akwapa tiba mbadala Na adui mkubwa wa zinaa (lakini alikufa kwa ngoma) Amsha akili janga kangha gani ulibebebee Siwaambii msiusie sisemi zipu mfungue Sisemi muache kuwa wema ila ujinga usiendelee Kwamba kila anayekufa kwa ngoma msidhani kicheche Tuamini bado ni wenzetu msiache wagonjwa wajifiche Hakuonekana na binti hakuwahi kuiasi dini Mfuasi wa maadili iiih (Lakini alikufa kwa ngoma) Alirudisha waliopotea akwapa tiba mbadala Adui wa zinaa iiih (lakini alikufa kwa ngoma Au sio, tumeelewana naamini, tusihukumu Hatuna hakina kuwa waathirika wana hatia Tusiwanyenyepaee... aaight