Hardward blood The personality change, yeah, hii ya leo hii! Hermy Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza) Unasema? (Bado nipo nipo sana) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mwana) Eeh? (Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!?) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mama) Unasema? (Bado nipo nipo sana) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza) Eeh! (Wa kuoa ntakuwa mimi mama!?) Japo natokea Tanga mapenzi yalipozaliwa Sijivishi ufundi nikajifanya nayajua Mi' nna akili timamu naona tu mnavyoyarukia Ukiniona na demu mzuri haimaanishi ndio ntamuoa Napata wakati mgumu washkaji wanapolia kwa uchungu Kwani na mi' n'na maumivu yangu nasema tu na moyo wangu Watu wanalalamika wanavyoumizwa na ndoa zao Wengine wanaficha wanakufa na maumivu yao Sioi leo, sioi keshokutwa wala mtondogoo Sioi mchana, sioi jioni, usiku wala majogoo Morale niliyonayo sasa siwezi kubali kuibiwa Ngoja nizeekezeeke kwanza pengine ntakuja elewa Eti nizibe maskio, wengine nifumbe macho Nisione wakati naibiwa? Hamuwezi kuwa hamjalewa Mi' nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi So miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza) Unasema? (Bado nipo nipo sana) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mwana) Eeh? (Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!?) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mama) Unasema? (Bado nipo nipo sana) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza) Eeh? (Wa kuoa ntakuwa mimi mama!?) Hata nikitaka kuoa niambie ntamuoa nani? Watu wana watu wao wengine toka zamani Ukiambiwa we ni boyfriend haimaanishi uko peke yako Wadogo usoni wanahifadhi wazee wako Sijui ni dhiki au tamaa tu? Watoto wanaanika njaa tu Hawafikirii mapenzi wanachoona wao ni mkwanja tu Msinipe headache staki kufuata mkumbo Nyi' anzeni mi' niacheni, sitaki kufanya gamble Marafiki wanauzana, ndio zao vicheche Na daima wanateteana, usiwaamini usiniangushe Anataka kuolewa na anamegwa kama kawa Demu wako akiuza wenzake, zinduka nae analiwa (yes) Sitaki kuoa sababu sitaki kulia Najipanga nisiharibu sitaki mje kunihurumia Nafahamu nina bahati mbaya kama nalala na bundi Ndio maana sijipi moyo wala sijitii maufundi Aliyelala na bibi harusi, siku moja kabla ya harusi Na wala sio bwana harusi, bado mnanishauri harusi? Eti, nizibe maskio wengine nifumbe macho Nisione wakati naibiwa? Hamuwezi kuwa hamjalewa Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza) Unasema? (Bado nipo nipo sana) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mwana) Eeh? (Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!?) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mama) Unasema? (Bado nipo nipo sana) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza) Eeh? (Wa kuoa ntakuwa mimi mama!?) Usiseme unaamini mwanamke hata kama unamtania Watu na akili zao washajichuuza na wakalia Sikatazi watu kuoa Na hata nikiwakataza neno langu sio sheria Sipendi wanawake napenda wanawake wazuri Wanaojitunza, wanajiheshimu sio wa simu na gari Inahitaji muda kuwapata hakuna anaewajua vizuri Ndio maana mi' nipo nipo sitaki kuvamia shari Wanatoroka na wazungu, wanamegwa na vibabu Wanaiba waume za wenzao uso mkavu hawana aibu Ukitaka wako peke yako labda umuumbe mwenyewe Au kata mgonjwa uufiche mtaani usishindaniwe Wakikumegea demu wako nawe tafuta mnyonge ummegee Haipunguzi maumivu inarudisha hadhi ya kiume Kumegewa ni jambo moja kukimbiwa ushafikiria? Sio kila demu umuonae unaweza kuoa Eti nizibe maskio! Wengine nifumbe macho! Nisione wakati naibiwa? Hamuwezi kuwa hamjalewa Mi' nikiona mtu anaibiwa naona kama naibiwa mimi! Sio miaka kadhaa ijayo ndio mniulize naoa lini! Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza) Unasema? (Bado nipo nipo sana) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mwana) Eeh? (Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!?) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mama) Unasema? (Bado nipo nipo sana) Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza) Eeh? (Wa kuoa ntakuwa mimi mama!?) Yes, yes, it's yo' boy FA Na Hermy B ni kazi chafu but lazima mtu aifanye! Sipendi wanawake napenda wanawake wazuri! Wanaojitunza, wanajiheshimu sio wa mkwanja na gari! Yeah, love is love my people Ladies, behave basi au sio?