Kishore Kumar Hits

Solomon Mukubwa - Nimewasamehe lyrics

Artist: Solomon Mukubwa

album: Habari Njema


Mmmh ...Ooh, oooh,
Nilipokuwa mtoto,
Nilizaliwa kama wewe,
Viungo vyote vya mwili,
Vilikuwa kama wewe,
Ghafla dunia, mambo yakageuka,
Nikajikuta kiugo kimoja, kimeniondokea,
Mimi nikajua kuwa, mwisho wa mambo yote
Imefika,
Wala sifai, nikaona dunia imenitupa,
Nikaona dunia imenidharau,
Nikajidharau mwenyewe nikajua sasa mimi,
Sifai tena, niliwanung'unikia,
Wote waliohusika, kwa haya mambo,
Roho ya kisasi ikaja juu yangu,
Nikajua sasa na mimi, nitalipa kisasi,
Kumbe kunaye mungu, mungu wa visasi
Akaniambia, Solomon nina mpango na wewe,
Lazima piga hatua, uwasamehe kwanza,
Ooh nikabishana na mungu,
Wote walionitendea mabaya,
Mimi siwezi wasamehe,
Moyoni mwangu, bwana kaniambia,
Wataka nitumike na wewe,
Nina ahadi zuri na wewe,
Kuhusu dunia hii ukitaka nitumike na wewe,
Uwaachilie wote, uliowaweka moyoni mwako,
Nikapiga hatua nikawasamehe,
Wote walionikosea
Bwana katumika na mimi ooh
(Refrain)
Nimewasamehe wote)x2,
Nimewasamehe kutoka moyoni mwangu,
(Nimewachilia wote)x2,
Nimewachilia kutoka moyoni mwangu x2
Tumekunywa damu, damu ya yesu,
Tumekula na mwili wa yesu ooh,
Mwili wa yesu ni msamaha,
Aah tujikane wenyewe,
Mara nyingi tumeonekana wajinga duniani,
Dunia imeshindwa kutuelewa wakristo, eeh
Umetendewa mabaya, lakini neno linasema,
Kubali nenda ukaombe msamaha,
Ki kawaida ya dunia,
Ukinitendea mabaya lazima ooh ieleweke,
Lakini kwetu sisi wakristo,
Ukinitendea mabaya, mimi lazima nikusamehe,
Sababu nisipokusamehe
Baba yetu wa mbinguni,
Na yeye hawezi nisamehe,
Haijalishi unapitia nini,
Kama wewe umeokoka,
Huwasamehe waliokukosea ooh eeh
Husifanye moyo walo jela,
Kuwafungia watu, amua leo uwaondoe,
Ili mungu wetu akubariki,
Samehe jirani yako,
Mungu na yeye atakusamehe
(Refrain)
Ni vigumu jamani mara nyingi,
Kuna mambo ambayo tunapitia,
Mwenzako mwanadamu anakupitisha kwa
Mambo mazito,
Lakini, unapaswa hufanyeje,
Ashurukuriwe mungu sababu neno la mungu
Linasema tusamehe tu,
Na tumevaa mwili wa yesu,
Tumekunywa damu ya yesu,
Kumbuka msalabani,
Yesu aliwaponya watu,
Viwete wakatembea mabubu wakaongea,
Akawalisha watu, zaidi ya elfu tano,
Lakini wale watu ndio walimuweka msalabani,
Mwisho msalabani ikasema baba wasamehe,
Huwasamehe,, kumbuka stephano,
Stephano alikuwa anapigwa mawe,
Alipokuwa anapigwa mawe, bibilia inasema,
Stephano kaambia baba huwasamehe,
Maana hawajui wanalolitenda bibilia inasema
Stephano akaona mbingu zinafunguka,
Kwenye msamaha kuna nguvu,
Kwenye msamaha kuna uwezo,
Stephano hakujali tena mawe wanayomtupia, wanayomchapa
Lakini stephano alikuwa ameona mbingu
Zimefunguka,
Na tayari anakwenda kupokelewa,
Msamahe jirani yako,
Kusudi uone mkona wa mungu,
Husimfungie kwenye moyo wako,
Utakuwa umujizuilia baraka yako,
Msamehe muachilie tu,
Maana tumevaa mwili wa yesu,
Na tumekunywa damu ya yesu,
Ooh yesu tusaidie kuwasamehe waliotukosea
Pengine una watu,
Ambao umefungia moyoni wala hutaki
Kuwasamehe,
Nakwambia leo, fungua moyo wako,
Ili mungu wa mbinguni akusamehae,
Husijiwekelee vikwazo,
Maisha ni mafupi yesu yu karibu kuja,
Huwasamehe wote waliokukosea,
Ili uone mbingu ooh, hatujui ya kesho,
Ya kesho ni ya mungu,
Fungua moyo wako leo, yule uliye mkopa hela,
Kashindwa kurudisha, sasa leo amekutusi,
Na yeye umsamehe,
Uwe safi mbele ya mungu yesu yu karibu kuja
(Refrain)

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

Similar artists