Kishore Kumar Hits

Sabah Salum - Ufukweni Mwa Bahari lyrics

Artist: Sabah Salum

album: Kwa Raha Zangu Taarab


Siku uliyotokeza roho umeichukua
Macho yanielekeza kwako wewe msifiwa
Siku uliyotokeza roho umeichukua
Macho yanielekeza kwako wewe msifiwa
Na moyo wanihimiza dhamiri yako kujua
Na moyo wanihimiza dhamiri yako kujua
Jinsi ulivopendeza sadiki nimevutiwa
Jinsi ulivopendeza sadiki nimevutiwa
Jinsi ulivopendeza sadiki nimevutiwa
Jinsi ulivopendeza sadiki nimevutiwaaah
Ufukweni mwa bahari mikono tumeshikanaaa
Mawimbi yameshamiri upepo umeumanaa
Ufukweni mwa bahari mikono tumeshikanaaa
Mawimbi yameshamiri upepo umeumanaa
Kwa vyovyote mi tayari
Hata tukijulikana kwa vyovyote mi tayari tena wataumwa sanaaa
Kwa vyovyote mi tayari
Hata tukijulikana kwa vyovyote mi tayari tena wataumwa sanaaa

Nimeshatua mahali
Mapenzi nishaibua
Bora haisomi hali
Muhibu ukanielewa
Nimeshatua mahali
Mapenzi nishaibua
Bora haisomi hali
Muhibu ukanielewa
Minampenda kikweli watu woote wanajuaa
Minampenda kikweli watu woote wanajuaa
Twaendelea wawili soote tushapendezewa
Twaendelea wawili soote tushapendezewa
Twaendelea wawili soote tushapendezewa
Twaendelea wawili soote tushapendezewa
Ufukweni mwa bahari mikono tumeshikana
Mawimbi yameshamiri upepo umeumana
Ufukweni mwa bahari mikono tumeshikana
Mawimbi yameshamiri upepo umeumana
Kwa vyovyote mi tayari
Hata tukijulikana
Kwa vyovyote mi tayari
Tena wataumwa sana
Kwa vyovyote mi tayari
Hata tukijulikana
Kwa vyovyote mi tayari
Tena wataumwa sana

Nyoyo tumezifungua
Wenyewe twajizuzua
Wenyewe twajizuzua waovu watajeua sisi tumejizingua
Nyoyo tumezifungua
Wenyewe twajizuzua
Wenyewe twajizuzua waovu watajeua sisi tumejizingua
Mimi na yeye murua kwa waridi na vilua
Mimi na yeye murua kwa waridi na vilua
Tena tumeshaamua na liwe litalo kuwa
Tena tumeshaamua na liwe litalo kuwa
Tena tumeshaamua na liwe litalo kuwa
Tena tumeshaamua na liwe litalo kuwa
Ufukweni mwa bahari mikono tumeshikana
Mawimbi yameshamiri upepo umeumana
Ufukweni mwa bahari mikono tumeshikana
Mawimbi yameshamiri upepo umeumana
Kwa vyovyote mi tayari
Hata tukijulikana
Kwa vyovyote mi tayari
Tena wataumwa sana
Kwa vyovyote mi tayari
Hata tukijulikana
Kwa vyovyote mi tayari
Tena wataumwa sana

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

Similar artists