Kishore Kumar Hits

Jahazi Modern Taarab - Nakula Kwa Nakshi lyrics

Artist: Jahazi Modern Taarab

album: Kazi Ya Mungu Haiingiliwi


Maa shaa Allah, Maa shaa Allah
Mtoto huyu Maa shaa Allah, ameumbwa;ameumbika.
Mtoto huyu Aaah,mtoto huyu Maa shaa Allah
Sifa na tabia zake,Mungu kamtunukiaa
Umbile na Sura yake,kidole na'katikia
Wenye kuumwa na waumwe,
Wenye kuchomwa na Wachomwe
Huyu ni wa kawangu mie lazima mnichukie,mnichukie
Kwetu hamzimi;hamuwashi
Tunakula kwa nakshi nakshi...
Yanasemwa mengi kuhusu mapenzi hayaaa...
Yasiyo ya msingi,lengo kutuchafuliaa...
Aaaaaah,hata mtafute taini,yakuja kutupekua
Aaaaaah,basi siri ya mtungi, kata tu ndio inajua
Jama ubaya haujengi, na hautawasaidia
Jueni hafi stelingi mpaka mchezo kuishia
Jamani kupendana raha,kupendana raha walimwegu msisikie...
Twajidai hadi raha,Oooh hadi raha jamani msinisogelee...
Kwenye raha tunaishi,kama hatupo duniani
Nakula kwa nakshi nakshi twaogelea pendoni
Mtoto huyu mcheshii,Mungu kanitunikia
Ameumbika ki-nakshi mtajiju mnao umia
Aaaaah,kwa Mungu fitina maleishi hayawi mnotegemea.
Aaaaah,mana mmezidi uzishi,pia kutufatilia
Mimi nikila kinashki vipi nyie mwaumia
Mimi na honey tunaishi kwa raha katika dunia
Jamani kupendana raha walimwegu msisikie
Twajidai hadi raha Ooooh hadi raha fisadi msitusogele
Kwenye raha tunaishi,kama hatupo duniani
Nakula kwa nakshi nakshi twaogelea pendoni
Labda aamue Mola,na In shaa Allah atalivua
Lakini kwa zenu hila puani zitawatokea
Nikitamani masala kimwana hunitengenezea
Au chapati na shira, hapo ndo ninapo mzimia
Mengine kusema ni hila nisije kumtibua
Mimi kwa nakshi nakula,poleni mnao umia
Jamani kupendana raha,kupendana raha walimwegu msisikie
Twajidai hadi raha, Ooooh hadi raha fisadi msitusogele
Kwenye raha tunaishi,kama hatupo duniani
Nakula kwa nakshi nakshi naogelea pendoni
Ya Mwisho:
Chuzi limekolea,haonjeshwi mtu.Utamu umezidia hapa hampati kitu
Imbeni nyimbo zote na vina mpangilie,
Simpi mtu yoyote hata machozi alie
Niko tayari kwa lolote,afe au nife mie
Chuzi limekolea,haonjeshwi mtu.Utamu umezidia hapa hampati kitu
Kama Simba wa mwituni mimi ndio nyama yake
Ikiwa yeye shetani hichi ndicho kiti chake
Akishapanda kichwani nitampa chano chake
Nipe nnachotaka kwako hunie,nipe nipe nnachotaka kwako Babe
Nipe nnachotaka kwako hunie,nipe nipe nnachotaka kwako Babe,niiiiiipe
Mwisho

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

Similar artists