Kishore Kumar Hits

Jahazi Modern Taarab - Shukrani Ya Punda lyrics

Artist: Jahazi Modern Taarab

album: Kazi Ya Mungu Haiingiliwi


Shukrani ya punda-JAHAZI MODERN TAARAB
Oooh aaah
Oooh
Wahenga wameona mbali sana, Ya kuwa punda shukrani hana
Na haya yamenipata, Leo Mimi nayaona
Kiumbe mbebe uwezavyo, Katu hatotulizana
Kweli binadamu, Tumekosa uungwana
Instrumental...
VERS: 1
Oooh aaah
Tenda wema uende zako shukrani usingoje
Si lazima wema wako ulotenda uuongoje
Tenda wema nenda zako shukrani usingoje
Si lazima wema wako ulotenda uuongoje
Jua mja hana shukrani, hili linajulikana
Hata umtendee nini, Pia shukrani hana
Bora fuga mbwa ndani, Mwaweza saidiana
Kuliko ya hiisani, Mtakuja kugombana
Bora fuga mbwa ndani, mwaweza saidiana
Kuliko ya hiisani, Mtakuja kugombana
Wako waja wana shukrani ya punda
Wako waja wana shukrani ya punda
Shukrani ya punda mateke, ya punda mateke
Ndo wafanyavyo, wafanyavyo
Mwenye uungwana wake, uungwana wake
Hafanyi hivyo, hafanyi hivyo
Hukumbuka wahisani wake, wahisani wake
Ndivyo ilivyo, ndivyo ilivyo
Instrumental...
VERS: 2
Aaah ooooh
Oooh aaah
Kwa nililowafanyia kwa imani, mmeyaapa kisogo
Safi yangu nia, toka moyoni
Mmeyafunga virago×2
Shukrani zenu, hazina mkia
Wa kuwaoongoza, muendako
Niliyoyafanya, kwa kujitutumua
Yote mmeyatupa huko
Bado mwanisilibia, Na kuongeza vituko
Mola atanilipia, Madhali sipo mlipo
Bado mwanisilibia, na kuongeza vituko
Mola atanilipia, madhali sipo mlipo
Duniani tends wema usisubiri malipo×2
Shukrani ya punda mateke, ya punda mateke
Ndo wafanyavyo, wafanyavyo
Mwenye uungwana wake, uungwana wake
Hafanyi hivyo, hafanyi hivyo
Hukumbuka wahisani wake, wahisani wake
Ndivyo ilivyo, ndivyo ilivyo
Instrumental
VERS: 3
Ooooh aaah
Aaah oooh
Sana inauma ufanye wema, shukrani usipewe
Tena inachoma yote mema, laawamani utiwe×2
Katu sikati tamaa, kutenda mema kwa waja
Mola ndiye anayejua, matendo ya kila mja
Mimi kimya nnakaa, sitopenda kujifuja
Nataka kuendelea, na wema wangu kwa waja
Mimi kimya nnakaa, sitopenda kujifuja
Nataka kuendelea, na wema wangu kwa waja
Shukrani ya punda kweli mateke×2
Shukrani ya punda mateke, ya punda mateke
Ndo wafanyavyo, wafanyavyo
Mwenye uungwana wake, uungwana wake
Hafanyi hivyo, hafanyi hivyo
Hukumbuka wahisani wake, wahisani wake
Ndivyo ilivyo, ndivyo ilivyo
Intro
Tenda wema kwangu nia, shukrani usitendewe
Ubaya utaambulia, wema wako ufungiwe
Roho haitataharuki, kutenda wema kwenu nyie
Wema hakupata nyuki, iweje nipate mie
Tenda wema kwangu nia, shukrani usitendewe
Ubaya utaambulia, wema wako ufungiwe
Mshipa haunitoki kukosa shukrani zenu
Kwangu mambo la msingi, siyafati yaloyenu
Tenda wema kwangu nia, shukrani usitendewe
Ubaya utaambulia, wema wako ufungiwe...

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

Similar artists