Maisha shida, kwako huwezi pika
Nyumba shida, kwako huwezi lala
Hayo yote ushuhuda,
Mungu anakutengenezea, mwisho ushinde,
Mambo unapitia, yanakufanya uzimie,
Yanakufanya we ulie, unajiuliza ako wapi,
Huyu mungu, wamuita kila siku
Huyu mungu, mi najua anasikia,
Huyu mungu anakupenda wewe sana,
Ila bado, mbingu husikia,
Tena bado mbingu itajibu,
Ila bado mbingu huelewa,
Tena bado mbingu itajibu,
(Basi wacha sasa iwe,
Vile mungu anataka iwe, mapenzi yake yawe, vile anataka yawe)×2
Kuna wakati, mbingu hunyamaza kimya,
Kuna wakati, mungu hunyamaza kimya,
Unaita ni kama husikiki, unabisha, wala hufunguliwi,
Unauliza maswali wala hujibiwi,
Ila bado, mbingu husikia,
Tena bado mbingu itajibu,
Ila bado mbingu huelewa,
Tena bado mbingu itajibu,
(Basi wacha sasa iwe,
Vile mungu anataka iwe, mapenzi yake yawe, vile anataka yawe)×2
Namuita mungu we hajafika,
Namlilia mungu we, akuhurumie,
Umepigwa hadi ukaenda chini,
Hauwezi inuka, unaonewa sana na kukanyagiwa,
Umefika mwisho we,
Sasa surrender dear
Mungu yuko nawe, tena karibu sana nawe eh,
Acha vita upiganiwe, acha mizigo ubebewe,
Siku yako itafika, basi wacha iwe,
(Basi wacha sasa iwe,
Vile mungu anataka iwe, mapenzi yake yawe, vile anataka yawe)×2
Iwe eh, iwe eh
Yawe eh, yawe eh
Поcмотреть все песни артиста