Ee Bwana Yesu niko mbele zako Baba Ninakuomba Baba unisikie Nahitaji nikujue, niyajue maneno yako Yesu Sheria zako Mungu zikae ndani yangu Uliwaambia Israeli wazishike sheria zako Bwana Kusudi baraka zako ziwe juu yangu Unishike nisipotee nikaenda kwenye njia isiyofaa Nikaliacha neno likapotea Unilinde mguu wangu nisifuate mabaya Adui asinimeze nikaangamia Huduma yangu mimi, utumishi wangu mimi Popote napohudumu nikuinue Yesu Nikumbushe ulikonitoa, ni mengi umenitendea mimi Nisije nikasahau wema wako Mungu Mimi nikae miguuni pako Ninaomba Baba unifundishe Roho wa Mungu mwalimu mwema Ninaomba Baba unifundishe Mimi nikae miguuni pako Ninaomba Baba unifundishe Roho wa Mungu mwalimu mwema Ninaomba Baba unifundishe Utusamehe watumishi, mara nyingi tumekukosea Baba Tunavyojiinua na tunakusahau Miujiza ikitendeka Tunasema ni kwa nguvu zetu sisi Tunasahau kwamba ni wewe umetenda Tunatumia madhabahu, kuyakuza majina yetu sisi Badala ya kulikuza jina lako Yesu Tumesahau mapatano, tulikuahidi ukituinua Baba Tutakuinua Yesu mataifa wakujue Hata sisi watumishi Tumeshindwa kuzifuata amri zako Tunatamani sana kulirekebisha neno Na kama ungeturuhusu, tuweze kulirekebisha neno Kila mtu angejiongoza anavyotaka yeye Tunafanya mazingaombwe, kwenye madhabahu yako Yesu Tunadhani tunaweza kukusaidia Mungu Tunapiga sarakasi nyingi Madhabahuni pako Baba Tunadhani tunaweza kukusaidia Mungu Lakini mimi nikae miguuni pako Ninaomba Baba unifundishe Roho wa Mungu mwalimu mwema Ninaomba Baba unifundishe Mimi nikae miguuni pako Ninaomba Baba unifundishe Roho wa Mungu mwalimu mwema Ninaomba Baba unifundishe Mimi nikae miguuni pako Ninaomba Baba unifundishe Roho wa Mungu mwalimu mwema Ninaomba Baba unifundishe Mimi nikae miguuni pako Ninaomba Baba unifundishe Roho wa Mungu mwalimu mwema Ninaomba Baba unifundishe Mimi nikae miguuni pako Ninaomba Baba unifundishe Roho wa Mungu mwalimu mwema Ninaomba Baba unifundishe Mimi nikae miguuni pako Ninaomba Baba unifundishe Roho wa Mungu mwalimu mwema Ninaomba Baba unifundishe