Kishore Kumar Hits

Bahati Bukuku - Barthimayo lyrics

Artist: Bahati Bukuku

album: Nimesamehewa Dhabi


Barthimayo kipofu aliketi kando ya njia
Akisubili wapitaji ili wamuhurumie.
Yesu alipopita ndipo kamuhurumia
Historia ya maisha yake yote ilibadilikaaaa.
Asante Bwana kwa kubadilisha historia ya maisha yangu
Ninakumbuka agano la moyo wangu
Ninakumbuka agano langu mimi na wewe,hasa nilipokutana na wewe Yesu
Uinuliwe jina lako baba
Bado ninanyenyekea chini yako
Bado ninakupenda wewe ni mwamba wangu
Yesu bado nakumbuka
Yesu bado nakumbuka agano la moyo wangu tangu nimekutana nawe.
Nilipo kutana na wewe
Nilipo kutana na wewe historia ya maisha yangu yote ilibadilika
Nilipo kutana na Yesu
Nilipo kutana na Yesu historia ya maisha yangu yote ilibadilika
Niliyekuwa maskini mimi
Niliyekuwa sina mali Ni Yesu wa huruma ndiye kaniwezesha
Niliyekuwa maskini mimi
Niliyekuwa sina mali Ni Yesu wa huruma ndiye kanishindia
Sioni haya mbele zako baba,bado nalitumainia jina lako
Wewe husinzii wala haulali
Siku zote bwana wewe ni mwema kwangu
Siioni haya mbele zako,siioni haya mbele zako
Wokofu niliyonao ndiyo najivunia mimi
Siioni haya kumtaja Yesu
Siioni haya kumsema Yesu mpenzi wa moyo wangu ameujaza moyo wangu
Siioni haya mbele zake
Shida zangu namwelezea Yesu rubani wa moyo wangu bado nakutumainia
Niliyekuwa maskini
Niliyekuwa nimehebeswa Yesu mpenzi wa moyo wangu sijajuta kuwa nawe
Mawimbi ni mazito,upepo ni mkali
Bado ninakutegemea,Bado najivunia uwokofu wako
Bado najivunia,furaha yangu ni neno lako
Asante Yesu asante unayetuliza mawimbi liinuliwe jina lako Baba.

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

Similar artists