Mmh, eh-eh-eh-eh
Ah-ah (ayo, Lizer) mmh
Ah-ah (Wasafi Records)
Wangu mtima, umeuchanachana
Ukaona haitoshi damu na hiyo ukanywa, eh
Mwenzako nasimamia kucha mama, eh
Mbona mapema umebadilika? Ai we, ai wewe, eh
Nateseka peke yangu (kwenye godoro)
Usiku ukirudi umelewa, eh (nakula kiporo)
Nahurumia moyo wangu (unabaki doro)
Mapenzi yaniua kihoroe (mmh)
Kusema ndio siwezi, nahisia kusema, "Inshallah"
Oh, mapenzi usiku ukifika nitalala, ai, ah-ah-ah-ah (ah)
Ah, ndo kwanza tupo kati ya safari yetu
Tuliyo panga tusonge mimi nawe, wewe
Nashangaa umekatisha zuri penzi letu
Umeniacha mwenyewe, wapi mi niende?
Ah, na mama nitamweleza nini? Maana nilishamwambia
Mwenzako umenikata ini, nyongo inaning'inia
Na baba nitamwambia nini?
Naye akija sikia, mwenzako umenikata ini, nyongo inaning'inia
Hali si shwari mwenzako naona maluweluwe
Kupendwa ugonjwa na kweli wataka uniuwe, eh, eh, hmm, ah-ah
Kipele, kipele kipele mwenzako kinawasha (ooh)
Naogopa kuropoka najua utaniacha
Usije kunibwaga jangwani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Mi kwako roho ita baki (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Bodaboda unipe urubani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Usipime penzi kwa mzani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
♪
Pale butcher nilipoisha nyama, likabaki shoka tu (hapo ndo mwanzo wa fujo zako)
Nilikua nimenona, nimebaki mifupa tu (chanzo mawazo sababu yako)
Kama kosa kupenda ni dhambi, kesho kwa mola nitakaa kitako nimuombe radhi
Ukisema unakwenda, basi nenda na moyo wangu, eh
Kweli penzi kilema niachie magongo yangu, weh
Sawa, chelewa kurudi nyumbani (bado hujanikomoa)
Ah, nitavumilia tu (bado hujanikomoa)
Eh-eh, nakupenda sana (bado hujanikomoa)
Kama sumu nishalamba panya (bado hujanikomoa)
Nimekuwa mlinzi na mgambo sijapitia
Unanikunisha nazi na kuosha masufuria, mm
Mchaka-mchaka moyo wangu naupeleka mbio kishenzi, natamani kusema basi, mm
Ila nashindwa kukufuta kwenye moyo wangu mwezako, nishadata nashindwa, eh, eh
Na, nahisi ujinga, eti leo nitake kuondoka wakati sijajenga nashindwa, eh, eh
Usije kunibwaga jangwani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Mi kwako hoi taabani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Bodaboda unipe urubani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Usipime penzi kwa mzani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Usije kunibwaga jangwani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Mi kwako hoi taabani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Bodaboda unipe urubani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Usipime penzi kwa mzani (basi, mama, basi, nanyenyekea)
Поcмотреть все песни артиста