Katika maisha yangu Nilipokea wageni Nikawakaribisha kwangu Wakafanya vitu vingi Hawakuwa wa kudumu Walikuwa wapitaji Ila moyo wa ukarimu Ukanisababishia machozi Mgeni wa kwanza alikuwa ni uchungu Akaniumiza, akanipa maumivu Alipomaliza akaenda zake Mgeni wa pili alikuwa ni huzuni Huyu naye Akanikosesha furaha Mgeni wa tatu alikuwa ni magonjwa Akanidhoofisha, akataka kuniua Hakufanikiwa akaenda zake Aliyefuata alininyima watoto Jina lake tasa Naye alipita Mgeni mmoja jina lake ni mauti Akamchukua Ntimi, akaniachia jeraha Mgeni mwingine jina lake hofu Hakutaka nifanikiwe Akanipa fikra potofu Nikajiona siwezi Tena nitafeli Huyo naye alipita Hawa ni wageni Tena wapitaji Hawatadumu, watapita Hawa ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita Hakuna jambo lolote gumu Litakalodumu kwenye maisha yako Ila yote yatapita Na yakishapita Hayatarudi tena Tough times never last But tough people do Mapito siyo mambo magumu unayoyapitia kwenye maisha yako Ila mapito ni mambo magumu yanayopita kwenye maisha yako Ndiyo maana ninaita mapito, kwa kuwa yanapita tu Na yanapita kwenye maisha yako, Na yakishapita hayawezi kurudi tena, ah Magonjwa, Hao ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita Uchungu, (Huzuni) Hao ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita Mateso, (Changamoto) Hao ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita (Hata dhiki) Hao ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita