Classic sounds (Mone...) Msodoki the son Classic sounds (Mone gangster) Kila mwanadamu anaupendo kwa yule ampendaye Mwingine anawaza vipi atampataje amtakaye Sio kwamba n'na-act, no nipo real Japo msodoki ni mdogo ila n'nauwezo wa ku-feel Fikra zangu zinanituma nidate kwa Maunda Zoro Najua nitaleta jealous kwa brother Banana Zoro Sasa vipi ningekuwa na Penny hivi n'takuwa free? Au kama ningekuwa na Mwasiti wa THT Ila Penny nahisi Diamond atanisumbua Hata Mwasiti najua pendo langu atalivua Kwanza long time ago nilishaga zimikaga na Wema Ila scandal za magazeti dah! Moyo wangu ukamtema Nikawachukia mapaparazi nikahisi wameharibu bahati Moyo wangu nikauweka bond kwa Chiku mwanaharakati Ila wote tunaachana hatudumu maghetoni Nilipozimika na Besta, Marlaw akapiga honi Madam Rita na Salama wakaogopa mcharuko wa BSS Nime-move mpaka Dar, Wolper nimchane face to face Ila roho inakataa inaogopa waigizaji Macho yalishatua kwa Flora, H-Baba akamhitaji Wapo wengi natamani kuwa nao in my life Muda mwingi natumia kuwaza nani ataenifaa Mrs superstar (nani?) Nani nimwite love? Mrs superstar (nani?) Nani nimwite love? Hizi hisia zangu sidhani kama nakufuru Akili inanituma niende sambamba na Lulu Ila naogopa yasinitokee ya Kanumba Nikasukumwa, nikafa, wengine wakang'oa mchumba Ama Ray C nikimcheki machoni haishi Kile kiuno bila mfupa kingenipikia mapishi Ila ghafla nikaogopa niliposikia ana mchizi Baada ya kuuliza ni nani? Kumbe m-Nako Lord Eyes Love kwa Pipi atanipa upendo wa kina Au tutaachana njia panda kama Amini na Lina Kwa love sitaki kukosea kuwa na mrembo mwenye visa Niwe na Tea au nimwache nidate kwa Monalisa Nikadata na Diva, ile sauti ni soo Ye' ndio mgonjwa kwa raha zangu atanifia, itakua soo Sura pesa Aunt Ezekiel, Young sina hela Vanesa Mdee najua hauwezi kuishi kisela Mara Jokate kichwani akanitawala mpaka basi Nikajua hata nikisema nahisi hatonipa nafasi Namuomba mungu anipe gift special Isingekua kizunguzungu basi ningekua na Rachel Wapo wengi natamani kuwa nao in my life (oh, oh, oh) Muda mwingi natumia kuwaza nani ataenifaa (baby) Mrs superstar (Mrs superstar) nani nimwite love? Mrs superstar (nani? Yeah, yeah) Nani nimwite love? (Mrs superstar) (Hizi hisia zangu Mrs superstar) Usiku silali usingizi hautokei Namuwaza Johari ila ule ukaribu na Ray Unanipa wasiwasi na'mi sitaki nijute Basi nikaamia kwa Dayna baada ya kusema nimvute Shilole naogopa kumwambia yanayonisibu Kwa Khadija nikakope kopa nije nimpe taratibu Nahisi atanihadhibu pedeshee wanafitina Maana atahitaji matunzo cha ajabu mimi uwezo sina Nampenda Uwoya mtoto wake ataniitaje Kaka au baba Ndikumana atanionaje Hizi hisia zangu wala siitaji maswali Mi' napenda kuitwa babu Bibi Cheka atakubali (oh, ooh) Wapo wengi natamani kuwa nao in my life Muda mwingi natumia kuwaza nani ataenifaa Mrs superstar (Mrs superstar) nani nimwite love? Mrs superstar (Mrs superstar, yeah, yeah) Nani nimwite love? (Mrs superstar) (Yeah, yeah) (Rudi mama, baby girl) (Rudi, nani? Baby)