Kishore Kumar Hits

Lava Lava - Ng'ari Ng'ari lyrics

Artist: Lava Lava

album: Ng'ari Ng'ari


(Ayolizer)

(Dopabeat)
Ah, nimetulizana ndege kwa kiota sitoki
Mambo mwororo
Nimenasiana hata kwa kukokotwa sing'oki
Kwa minyororo
Nishasahau zamani kushikana mashati mizozo
Mapenzi gani kila kukicha vibonzo
Nimepata mwandani bila VAT bila tozo
Wambea kunani mnakipi 'kina mama nyonzo
Na nimeamua sitaki sitaki
Kurudia matapishi, nishakula yamini divai
Aende akanishitaki mahakamani, polisi
Kama kuna kitu ananidai
Oh, poleni wanokonoko, penzi linametameta, meta
Mwali fundi si kitoto, kama kasomea VETA, VETA
Mwiteni na kiroboto, mje na matarumbeta, mbeta
Sisi twachochea moto, roho kuwakereketa
Penzi linang'ara, ng'ari ng'ari
Mtaliona hivi hivi, ng'ari ng'ari
Kwa mbali linapepea, ng'ari ng'ari
Mtaliona hivi hivi, ng'ari ng'ari
Wenyewe twajifaidia

Aniita, aniita mi' Ayuni
Namwita namwita Nyonda Sabuni
Anipa anipa mpaka bafuni
Sio mbwembwe ndio zake tamaduni
Ah, najiamini niko peke yangu, ndio maana natamba
Sina shaka hofu kwa raha zangu, hata mkinichamba
Wenye roho za kwanini, nitajijua zangu niko naye sambamba
Mi' napenda yake anapenda yangu, kuilamba lamba
Zifikisheni salamu kwa yule kidudu mtu
Mwambie kutesa kwa zamu asipige marufuku
Yani ni mashamu shamu leo mambo iko huku
Nimempata Beckham fundi si butubutu
Oh, poleni wanokonoko, penzi linametameta, meta
Mwali fundi si kitoto, kama kasomea VETA, VETA
Mwiteni na kiroboto, mje na matarumbeta, mbeta
Sisi twachochea moto, roho kuwakereketa
Penzi linang'ara, ng'ari ng'ari
Mtaliona hivi hivi, ng'ari ng'ari
Kwa mbali linapepea, ng'ari ng'ari
Mtaliona hivi hivi, ng'ari ng'ari
Wenyewe twajifaidia

Mwenzenu napewa vitamu; tende, halua, halua
Vya pwani, vya bara; tende, halua, halua
Anipa haninyimi wala; tende, halua, halua
Mwenzenu nalishwa nalala; tende, halua, halua
Aah

(Wasafi)

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

Similar artists