Kishore Kumar Hits

Mathias Walichupa - Navumilia lyrics

Artist: Mathias Walichupa

album: Navumilia


Unisikie BWANA
Maombi yangu nikuombayo
Uyafute kabisa
Na machozi yangu yanitokayo
Jibu lako kwangu ni muhimu kulisikia
Ni mwangaza wa njia zangu
Maisha yangu yanakamilishwa na wewe
Maana siwezi bila wewe
Macho yangu yakutazama wewe
Please please usiniache peke yangu BWANA
Navumilia vumilia yote yana mwisho
Navumilia vumilia yote yana mwisho
Siwezi kuacha kuvumilia, maana ninajua
Ni mbali nimetoka na hapa umenifikisha
Ndio maana kwako mi nimekimbilia
Sababu ninajua
Majibu yangu ni wewe utanipatia
Sisikii yale wanayo nisema sema
Kunikatisha tamaa
Kwako Bwana mimi nitangojea
Mimi naamini kwako Bwana ipo siku
Utanitendea Sikati tamaa
Navumilia vumilia yote yana mwisho
Navumilia vumilia yote yana mwisho
Navumilia vumilia yote yana mwisho
Navumilia vumilia yote yana mwisho

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

Similar artists