Kishore Kumar Hits

Roma Mkatoliki - Zimbabwe lyrics

Artist: Roma Mkatoliki

album: Zimbabwe


Instrunmental
Tongwe records
Bin laden
(Oooooh) Geof master (ooooh)
Wengi mlijiuliza walioniteka ni maaskari
Mkanitafuta vituo vyote central hadi Sitaki shari
Wakasema hawajui nilipo mama alienda hadi mortuary (dah!!)
Ya Kaisari muachie Kaisari,
Machozi yenu yatalipwa mi nafunga na kusali...
(Imba Roma imba, imba Roma imba, imba Roma imba)
Mungu wa Paulo, ndo Mungu ungu wa Daudi,
Na ndo Mungu wa John mnaemuita Yohana wayahudi
Mwanangu alimuuliza mama baba lini atarudi
Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sina budi
Fahamu ya kuwa mi sio tu rappa, mi ni baba wa familia
Na watoto mahitaji nawapa kama isemavyo biblia
Kipi bora? Nife mseme nilikufa kiharakati?
Siogopi kufa, ila nawaachaje wanaobaki?
Je, nani kati yenu mwanangu atampa malezi?
Wapi atapata mahitaji, wapi atapata mapenzi?
Mama nae wapi atapata mahitaji na malezi?
Na ripoti ya upelelezi vipi akiiteka mtekaji?
Je kaburi langu mtalipalilia majani?
Nimeumwa hamjakuja niona mnangoja mje msibani
Nilipokuwepo sikuwa najua hii saa nne, hii saa nane
Nilichohitaji nitoke mzima na ndugu zangu tuonane
Nimechapwa mijeredi, nimevunjwa bila huruma
Asante mliopaza sauti nmeiona nguvu ya umma
Siku tatu nimefungwa macho mikono
Imefungwa nyuma (mikono imefungwa nyuma)
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee.
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee.
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee.
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee.
Imba Roma imbaaa, eeeh Roma, sema baba weeeh
Nasimama na naunga hoja kwenye uchumi wa viwanda
Nanasi linaoza Msoga tikiti linaoza shamba
Waloniteka hawakuja na Noah, ni uvumi na visanga
Ila kutekana tekana huu ni uhuni wa kishamba
Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja
Maana sote lengo letu kuijenga Tanzania moja
Mi sikuona nyota kwa shoulder ila najua we ni soldier
Inshaallah, ulikuja mwenyewe au ulipewa order?
Aminini siku hazigandi, we ni Yanga mi Simba kuwa mpinzani sio dhambi
Ipo siku mtawala atakua mpinzani
Simba akichukia kombe sijui atapona nani
Na kuna mbunge alisema eti nimemtukana mkuu
Utahukumiwa na mkono wa Mungu
Namshitakia alie juu
Kwanza lini na kwann mi nimtukane mjomba
Umepewa gari ya wagonjwa mi tanga ananijengea bomba
Mi mbarikiwa na Nikifa kuume kwa baba ntaketi
Na mtu wa watu that's why lilisimama bunge la bajeti
Kunijadili mtanzania kuwa makini pia
Makinikia nayatungia mapini pia
Nilitabiri utaitwa raisi kipindi unaitwa waziri
Japo maisha sio rahisi ila pongezi unastahili
Na waliosadiki Roma ataonekana kabla ya
Jumapili God bless imetimia injiri niliyoitabiri
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee.
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee.
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee.
Nakwenda Zimbabwe, simama iyelele mama wee.
IMBA ROMA.
Eeeeeeh Roma, simama simama
Oyoyoyo eeeeeh Roma, (sema baba wee)
Iyelele mama wee, wee nakwenda... wee Zimbabwe
Iyelele mama wee, mama wee
Ooooh

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

K

2017 · single

Similar artists