Kishore Kumar Hits

Roma Mkatoliki - 2030 lyrics

Artist: Roma Mkatoliki

album: 2030


Instrunmental
Tanzania eeeeh (tongwe records)
Nchi yangu oooh
Huwezi kuijenga Roma, haikujengwa kwa siku moja
Iwe kwa raha leo au simba mtoto Tanga watakuja
Hata Patcho pia ni mwamba ila bado anakata viuno
Kaskazini bila Tanga ni msondo bila Gurumo
Alisema juu ya mwamba atalijenga kanisa na halitatikisika
Waumini tuianze misa
Kwenye njaa kula kuku aliechinjwa na padri awallah
Adhana ikilia amka ukamwombe Allah
Bwashee mrudie Mungu Masanja kawa mchungaji
Sujudu Makka madina tajiri hataki kuhiji
Maulidi Ubungo kibangu ndo mishahara ya madrasa
Ona rafiki wa padri kawa muhasibu wa kanisa
Tenda wanapeana kindugu mwanangu kua uyaone
Familia ilikata ringi na mama alibaki mjane
Sikuwa na damu ya kiarabu kwamba ntarithi mabasi
Dingi hakutupa msingi ona gari twaifanya taxi
Tazama Gongo la mboto mtoto kamzaa mtoto
Na atalelewa na nani baba ake mmemfunga keko
Wape buku waue winga wale watoto wa Morocco
Mungu atazidi kulinda kesho utaiona sabato
Mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani
Ana wake wake watatu je watoto watarithi nini
Ndo chanzo vha kurogana na kutupiana majini
Huyu akimpandisha makata hule maimuna subiah
Maana pesa ndo ilifanya tusiwe na Tanga ndugu
Pesa ilileta ubaguzi kati ya Loyola na Pugu
Pesa ndo ilichochea bifu ya Nice na Dudu
Na pesa ndo ilimaliza vita ya Ruge na Sugu
Tanzania eeeh
Mwanangu kua uyaone kama ntawahi kuiona paradiso mtunze mama ako
Nchi yangu oooh
Mwanangu kua uyaone marehemu hufa na chake pigana upate chako
Tanzania eeeeh
Mwanangu kua uyaone mwalimu cheza kibati wanao wasife njaa
Nchi yangu oooh
Mwanangu kua uyaone elimu imekosa thamani necta imevuja kibaha
Aminini nawaambieni ujana ni maji ya moto
Mtoto humzika mama leo mama anamzika mtoto
Ndo maana mama alisema nisimchumbie
Mmachame muraa shusha mapanga naileta posa Tarime
Leo bahari imechafuka mpemba iheshimu karafuu
Hatari kama Nungwi nahodha sio kirikou
Yahee nirushie mtumbwi
Me mwamba sio kichuguu
Hii ni vita ya msambaa mbodei usitie maguu
Ona kipindi cha bunge Dodoma inanuka ngono
Spika akiahirisha bunge wengi watausapoti mgomo
Wabunge mnadai posho, muhonge dada zetu
Kuna wanafunzi wa mama salma vyuoni usicheze peku
Wazanzibar hawaioni thamani ya huu muungano
Ila kulichoma kanisa sio njia ya kuvunja agano
Sioni sababu ya ubaguzi na kuua wasio na hatia
Wakati aliochanganya mchanga, mchanga umeshamfukia
Muislamu gani unahonga bongo movie mamilioni
Mama anakufa mwaisela kakosa drip ya quinine
Ni kheri ujenge msikiti tuitukuze mitume
Anasa za bakurutu unawatuza wacheza sebene
Unamuheshimu ramadhan unazini mbele ya shaban
Kama ilishushwa kuran twendeni misikitini
Anaedhihaki msaafu pengine kanisa halijui
So kulichoma kanisa ni kuuza bible Dubai
Usihofu kumpoteza mmoja ili kumi waishi vyema
Watanzania tuna uoga sio amani mnadanganywa
Sacrifice for your son and daughter amka kifikra
Damu yako iwe chachu ya ukombozi Dr Ulimboka
Mjinga usimuue mama ili uongeze kipato
Utajiri upo kaburini watu wamekufa na ndoto
Leo Ridhiwani hafanani na Makongoro
Dah sina hela ya kiroba Rashid nigongee ugoro
Suka kaiangusha lorry ya mafuta yote magendo
Waziri anaziuza pembe za ndovu na meno ya tembo
Nchi imejaa misitu tuna uhaba wa madawati
Tunakula vitu feki (what) TBS mko wapi
RPC usitume kikosi ili uishushe chadema
Italipwa damu ya Mwangosi Iringa semeni amina
Okoa wagonjwa wa saratani mpakani zuia wakimbizi
Kuliko kumwaga pesa kwenye tume za uchunguzi
Muhimbili naumwa goti eti dokta kapasua kichwa
Mbeya wanapigwa nyundo ili raia wauze mabucha
Amana wanatelekeza watoto wanalia
Mwananyamala wanatuua na hawaendi jela jela anaenda Kajala
Tanzania eeeeh
Mwanangu kua uyaone cashier acha kisirani ngonga muhuri tuwahi
Nchi yangu oooh
Mwanangu kua uyaone mnafki hasira za mkeo barabarani hazifai
Tanzania eeeeh
Mwanangu kua uyaone wanahonga mashabiki ngoma zao wazi repaste
Nchi yangu oooh
Mwanangu kua uyaone udini wa mapresenter wapagani unatukosti
Sauti hii itasikika mpaka Oldonyo lengai
Nikifa naomba nizikwe Tanga na mje kwa shambalai
You can tell me bro but won't kill what I'm standing for
Siutamani urithi wa baba ikimshuka CD 4
Eti tuzo sikustahili hahaaa hii ni hatari
Tuzo ina chapa ya nani ya kaisari mpe kaisari
Me sio masaki ni ngaramtoni mama anaiuza dadii
Muziki umejaa stress kila nyuma ina msanii (oyoooo)
Yanga wamemfukia mbuzi golini Simba wana bundi
Viongozi wanataka umate umate hawaujali ushindi
Utaskia Chuji kachuja jamhuri choma mahindi
Kapigwa ligi ya jogoo shahidi kamati ya ufundi
Vijijini tuko wengi mleteni daktari bingwa
Ana ngoma uyasikia karogwa twende kwa mganga
Pesa za kujikimu nd ulichongesha kitanda
Kulea mimba sio mchezo baba kijacho haujajipanga
Profesa kanyimwa penzi utaskia Calo kadisco
Na Caro analea ndg kwe pesa ya bodi ya mikopo
Pole mnaotafuta C mwaka wa nne mnarisiti
Huku headmaster kaenda mjini eti shule imeiahiwa chaki
Msiwaue wachimbaji wadogo Geita inalia
Kaburu umempa migodi UDSM tuna engineer
Unapewa kontena la kondom uihonge dhahabu
MV spice ilipozama TV inaonesha taarabu
Kamanga hawaiweki lami ili tuvukie Busisi
Dereva usinitoe kafara ili utimize hesabu ya bosi
Sina cha kuweka rehani kwenye asasi za mikopo
Bajeti ya kilimo kwanza mkulima silioni soko
Tanga mmekosa nini amkeni acheni umwinyi
Hawa wachaga hawatuwezi ona Manka balaishirini
Bandari chanu railway chali Makamba iinue katani
Zitto akirogea Kasuru si tunamrogea Pangani
Uchafu wa Mrisho unafanya msafi aonekane Benja
Sisadiki magazeti waandishi wengi kanjanja
Vijana ndo nguvukazi ila wengi wamejali utindi
Mtaani wamekata ringi haki msingi wanaziweka bond
Majibu ya postmortem kashanunua wakili na
Hakimu kapewa kiwanja kimara apige kufuri
Cheki dola wanainunua kesi napewa kapuku
Nna upole kama ngamia mbele ya hakimu wa kisutu
Tanzania eeeeh
Mwanangu kua uyaone
Nchi yangu oooh

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

K

2017 · single

Similar artists