Kishore Kumar Hits

Stamina Shorwebwenzi - Machozi lyrics

Artist: Stamina Shorwebwenzi

album: Machozi


(SMG)
(Paradise Music)
Oy, niaje mwamba samahani nakusumbua
Naomba usikate simu taratibu utanijua
Nampigia mke wangu naona hapokei simu
Ila najua umelala nae, sorry na kukata stimu
Na unanijua, na unajua si' ni wazazi
Naumia kuona wanangu wanalala na dada wa kazi
Na usiulize namba yako nimeitoa wapi
Naomba u'siki'ze mi' ni mmewe wa ndoa na sio mchati
Kwanza nikupe pongezi, we' mjasiri!
Mi' kulala na mke wa mtu siwezi
Unapata nguvu ipi kujipa hayo mamlaka
Angali mume wake yu' hai hajafa hajampa talaka
Halafu nas'kia una-sound umechoka sana
Na mshamaliza round ya kwanza au sio mwana
Wakati mimi nalalia mito
We una-enjoy tu, unamkunja kama kiko
Vipi mtamu eh!? Kanona eh!?
Nagharamika bro, sijui kama unanisoma, aisee
Najua unampenda sababu unamhudumia
Ukitaka nikuachie bro uone jinsi nnavyoumia
Kama kidume cha mbegu kesho nikuletee watoto uwalee
Na mke wangu unipunguzie msoto
Inaniuma nimehudumia nimempa thamani zamani
Nakuhakikishia ungemwona usingemtamani
Kama anasema ndoa imekuwa, dah! Changamoto
Au anasema tumeachana nimebaki nnalea watoto
Sorry, salio linakata nnaweka vocha nakupigia
Ili unipe simu niongee na huyo mshenzi wa tabia
Kama binadamu n'na moyo sio chuma, naumia
Machozi yanitoka nashindwa vumilia
Natamani niondoke hata kwenye hii dunia
Maana heshima yangu we' umeshindwa nitunzia
Unaniumiza moyo (eh)
Akili yangu haisomi (eh)
Umenishusha thamani (eh)
Nadharaulika mtaani (eh)

(Hello)
Pole sana kwa uchovu
Pole kwa kazi nzito ya kubeba pembe ya ndovu
Najua ulipanga unidanganye boya lako
Kuwa party iliisha late ukalala kwa shosti yako
Kukuita malaya sitaweza
Umenizalia watoto ila heshima unaipoteza
Japo mambo unayofanya kiasherati, we sio smart
Umesahau una familia au na watoto huwataki
Okay tuseme sikuridhishi kitandani
Je anayetoa kodi ya meza hapa nyumbani ni nani?
Unadhani watoto watakula tu sex yetu
Au nikikosa hela watalishwa na bwana yesu
Zile make-up, kusuka, wanja, saluni
Ungezipata wapi nisingekaza kisabuni?
Hata kama sio handsome nilitimiza majukumu
Sa' huyu atakupa nini zaidi ya kukulisha ndumu?
Wazazi waliposema kuwa tukapime DNA
Nilisema, "Wamezeeka hawa wazazi TZA"
Sa'hivi naelewa kila nikiwacheki watoto, sura yangu
Inakuja, inaondoka, changamoto
Ukirudi nyumbani chukua kilicho chako
Tena ikibidi nenda na watoto wako
Nauonea huruma huo mfuko wako wa uzazi
Ungekuwa mfuko wa kawaida ningeshaubebea viazi
Kama binadamu n'na moyo sio chuma, naumia
Machozi yanitoka nashindwa vumilia
Natamani niondoke hata kwenye hii dunia
Maana heshima yangu we' umeshindwa nitunzia
Unaniumiza moyo (eh)
Akili yangu haisomi (eh)
Umenishusha thamani (eh)
Nadharaulika mtaani (eh)
Ah-a-ah
(SMG)

Поcмотреть все песни артиста

Other albums by the artist

Similar artists