Killy Mbeya Iye iye iye iye iyeee iyee Iye iye iye iye iyeee iyee Aaah unaposkia neno ndoa(Ndoa)ujue noma Kabla kuongea chochote Naomba kwanza kusonya (Msschew...) Sijali nishauri nani aisee ok twende Aliyenifundisha mapenzi Hakuniambia kuhusu kuoa Alinionyesha staili za tendo Ila sio maisha ya ndoa Aliyesema ndoa ndoano Hivi huyu mjinga ni nani? Kafanya nivue samaki Kwenye bahari yenye tsunami Nikiziona picha za harusi Najiskia vibaya Namuonea huruma padri Pamoja na waimba choir Yale mafunzo ya katekista Eti yamepotea mazima Sadaka misa ya ndoa Bora mngewapa watoto yatima Pole wasimamizi wa ndoa Kwa ujinga mliosimamia Mngesimamia ukucha Mngekuza hata familia Kama ni pete Nisharudisha kwa sonara Tayari nishavuta mpunga Nimerudisha nusu hasara Kabla kuingia ndoani Anakuwa kondoo usiyemjua Ila ukimweka ndani Nyani anakuachia mabua Marafiki, mashemeji Ndio wanafiki nakuambia Wanaweza kufanya ulewe Bila hata kukupa bia Pre-chorus Sasa ile suti(Ilifanya ya nini?) Na mchango(Nilichangisha ya nini?) Na wale ndugu(Niliwaita wa nini?) Na kile kiapo(Niliapa kwa nini?) Naubembeleza upepo Usizime kibatari(Iye iye iye) Kichwani mwangu hayupo Moyoni niko shwari(Iye iye iye) Ona hajaacha pengo mwambie, asiwaze Huko aliko atulie, asiwaze Kama amepoteza lengo mwambie, asiwaze Huko aliko atulie, asiwaze Mwambieni yule dogo aliyeichezea club ya Simba Kutembea na mke wangu asijione kama ameshinda Mi samaki, mapenzi yangu yana chombo Kaka yake nishakula so ruksa kutoa vyombo Hata posa nililotoa mwambieni aingize vikoba Ila atakaye muoa ampe mtaji wa bodaboda Ama kweli hii dunia ina mambo mengi Na ndoa ni kama boti haiwezi kupaki stendi Hichi cheti cha ndoa nimebaki nacho kwa nini? Siwezi kuombea kazi hakina mchongo apa mjini Hata Biblia imeandika wanawake tuishi nao kwa akili Kwao sikumficha kitu ulimpa hadi sehemu za siri Akiskia nimekufa mwambieni asilie sana Aite rafiki wafurahi wachome nyama Nitazikwa na ndugu, rafiki na mafans kibao Mkimuona msibane nitafufuka nimzabe vibao Unaweza kumpakia mkongo mkeo na usimfikishe Alafu anayempakia mkorogo ndio akamfanya amridhishe Ndoa ndoana anayebisha aniulize mimi Nishawahi kuwa na mahusiano Ambayo sijui yanahusiana na nini Pre-chorus Na ile keki (Nilikata ya nini?) Na mahari (Nililipa kwa nini?) Na yule mshenga (Nilimtuma wa nini?) We si uliapa tena ukala yamini Naubembeleza upepo Usizime kibatalii (Iye iye iye) Kichwani mwangu hayupo Moyoni niko shwari (Iye iye iye) Ona hajaacha pengo mwambie, asiwaze Huko aliko atulie, asiwaze Kama amepoteza lengo mwambie, asiwaze Huko aliko atulie, asiwaze Wewe ambaye hujaolewa Usifanye kama hutaki kuolewa hivi eeh Alafu na wewe ambaye hujaoa Sio kwa sababu ya nyimbo Eti ukakata tamaa ya kuoa (Mmmh mmh) Sijasema hivo aiseee Asiwazee! Hata akinisema popote pale Asiwazee! Na hata tukionana mahala popote pale (Asiwaze) Bear, Peace! I live my life men Killy Records Lets take over the game