Niko fresh niko poa Asante Mungu kwa pumzi nayopumua Nakuombea mama umenileta kwenye dunia Leo utafurahi kidogo mi nawe tukiongea Kwanza pole kwa msiba baba ametangulia Najua una kazi nzito ya kuongoza familia Kabla baba kufariki kuna mambo yalitokea Wapo waliopenda wengine walichukia Mama huenda baba anajua ni ukoo moja Ila mama we na baba najua si kitu kimoja Umejaliwa hekima busara na upendo Inshallah tutafika mbali usipo badili mwenendo Kuna baba wadogo hawa kuwa nao makini Bado hawaamini kama ndo umeshika mpini Waongo wanafiki wamejawa ufitini Wanaongoja uteleze ili wakupige chini Hey mama we love you mama Hey mama tunakupenda sana Hey mama we love you mama Hey mama tunakupenda sana Tukificha maradhi kifo kitatuumbua Mama tusipoziba ufa hakika tutajenga ukuta Kuna mambo ya msingi ni lazima kuyaongea Mama sio kwa ubaya ni kujenga familia Baba alikuwa mkali mama mwenyewe unajua Yaani tuliishi kwa taabu japo kuwa ni wa kishua Sio sisi tu mpaka wageni walikimbia Kuhusu kaka yangu Ibra natumai ulisikia Naye alikimbia ameacha mke na watoto pia Wengine walipotea tu hatujua wako wapi? Sema neno kuhusu hili mama ututoe wasiwasi Mama njaa ikiuma tunaruhusiwa kusema Ukikosea tunaruhusiwa kuongea Au ndio kama baba mtu mzima hakosei? Nina zawadi yako siku yako ya birthday Hey mama we love you mama Hey mama tunakupenda sana Hey mama we love you mama Hey mama tunakupenda sana Mama hili la mwisho Najua unajua kwamba, ukishatengea na familia yako Huruhusiwi na unapoteza sifa za kushiriki kwenye vikao Vya maendeleo ya ukoo Lakini shangazi Halima na wenzake Mbona bado nawaona kwenye vikao vya ukoo? Na walishatengwa na familia yao? Sema kitu kuhusu hili mama All the best mama Wajukuu zako nyumbani wanasubiri Nirudi na chochote kitu Acha nikatafute Hey mama we love you mama Hey mama tunakupenda sana Hey mama we love you mama Hey mama tunakupenda sana