Siku nyingi binti namfukuzia Alishantosa nishakata tamaa Sikujua kama kwangu angekuja Nilitoa matumaini ya kumpata Siku nyingi binti namfukuzia Alishantosa nishakata tamaa Sikujua kama kwangu angekuja Nilitoa matumaini ya kumpata (Leo hii kaja mwenyewe mchumba) Ghetto kwangu mpaka ndani kaingia (Nilimuuliza naeza kukusaidia) Akacheka kisha akaniambia Ombi langu lile amenikubalia Siku zote alikuwa akinifikiria Niliruka kwa furaha kubwa sana Sikuamini kama mchumba ningempata (Usilojua ni usiku wa giza) Ningetambua bora ningemtimua (Usilojua ni usiku wa giza) Ningetambua bora ningemtimua Nani, ataniona mi ni mkweli? Nani nikimuelezea ataniamini? Nani, ataniona sio katili? Nani, atanisaidia mimi? Nani, ataniona mi ni mkweli? Nani nikimuelezea ataniamini? Nani, ataniona sio katili? Nani, atanisaidia mimi? Baada ya stori binti nilimuuliza Kinywaji gani angeweza kutumia Alinieleza kisha mi nikainuka Nikaelekea dukani kununua Baada ya stori binti nilimuuliza Kinywaji gani angeweza kutumia Alinieleza kisha mi nikainuka Nikaelekea dukani kununua (Huwezi amini nyuma nilipomuacha) Baada ya kurudi ndipo kizaa zaa (Binti alikuwa kitandani kajilaza) Nilimuamsha lakini hakuamka Pumzi zake zilikuwa zimekata Nilidhani labda kazimia Maji ya baridi kichwani nilimwagia Lakini hata hakushtuka (Kumbe alikuwa tayari ameshakufa) Nimekwisha Hussein bila kujua (Kumbe alikuwa tayari ameshakufa) Nimekwisha Machozi bila kujua Nani, ataniona mi ni mkweli? Nani nikimuelezea ataniamini? Nani, ataniona sio katili? Nani, atanisaidia mimi? Nani, ataniona mi ni mkweli? Nani nikimuelezea ataniamini? Nani, ataniona sio katili? Nani, atanisaidia mimi? Ee Mola, nimekosa nini? Ee Mola, niokoe mimi Ee Mola basi nipe akili Mimi nifanye nini Ee Mola, nimekosa nini? Ee Mola, niokoe mimi Ee Mola basi nipe akili Mimi nifanye nini Furaha yangu, imekuwa kilio changu (kilio changu) Furaha yangu, imekuwa kilio changu Ndoto zangu leo majonzi kwangu Ntawaeleza nini walimwengu? Ndoto zangu leo majonzi kwangu Ntawaeleza nini walimwengu? (Vipi, wataniona mi ni mkweli?) (Vipi nikiwaelezea wataniamini?) (Vipi, wataniona sio katili?) (Vipi, ingekuwa wewe ungefanya nini?) Nani, ataniona mi ni mkweli? Nani nikimuelezea ataniamini? Nani, ataniona sio katili? Nani, atanisaidia mimi? Nani, ataniona mi ni mkweli? Nani nikimuelezea ataniamini? Nani, ataniona sio katili? Nani, atanisaidia mimi?